May 24, 2018


Na George Mganga

Klabu ya Simba imekabidhiwa kitita cha shilingi milioni 100 na wadhamini wake, kampuni ya SportPesa, kama zawadi ya pongezi baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Kwa mujibu wa masharti ya mkataba walioingia na kampuni hiyo ya bahati nasibu, mojawapo ya kipengele kinaeleza kutoa kiasi hicho cha fedha endapo timu itafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi.

Hundi ya fedha hizo imetolewa leo na Mkurugenzi wa SportPesa nchini, Abbas Tarimba, kupitia kikao kilichoitishwa mbele ya Waandishi wa Habari katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Kwa ujumla klabu ya Simba inakuwa imejinyakulia kiasi cha milioni 180 ukijumlisha na zile za ubingwa wa ligi ambazo hutolewa na Mdhamini Mkuu, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom.

Kampuni ya Vodacom itawakabidhi Simba fedha zao kiasi cha milioni 80 mapema baada ya ubingwa wa ligi kumalizika.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic