May 16, 2018


Na George Mganga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia ombi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhudhuria hafla ya kuwakabidhi Simba SC kombe la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2017/18.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Ndug, Wilfred Kidao, Magufuli amekubali ombi hilo kufuatia barua iliyotumwa na Rais wa TFF, Ndug Wallace Karia kupitia kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ikiomba ugeni rasmi juu ya hafla hiyo.

Simba itakuwa inacheza na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Jumamosi ya wiki hii, Mei 19 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, ambapo mechi hiyo itaenda sambamba na mabingwa wapya wa ligi, Simba, kukabidhiwa kombe la Rais Magufuli.

Mbali na Simba, Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, itamkabidhi Rais Magufuli Kombe la CECAFA ililofanikiwa kulitwaa nchini Burundi baada ya kuifunga Somalia kwenye mchezo wa fainali, jumla ya mabao 2-0.

Sherehe za hafla hiyo zitaaza majira ya saa 8 kamili mchana huku mashabiki na wadau wote wa soka wakiombwa kufika mapema kabla ya Rais kuwasili Uwanjani ili waweze kujionea tukio zima litakavyoenda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic