May 23, 2018


Kamati ya Tuzo za VPL, imekamilisha orodha ya awali ya wachezaji 30 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msimu wa mwaka 2017/18, ambayo sherehe zake zitafanyika Juni 23 mwaka huu.

Kila mwezi Kamati ya Tuzo, imekuwa ikitangaza jina la mchezaji aliyefanya vizuri kwa mwezi husika kutokana na vigezo mbalimbali na pia ripoti kutoka kwa makocha waliopo katika viwanja ambavyo ligi hiyo inachezwa.

Wachezaji walioshinda tuzo za mwezi ligi ya msimu huu na miezi yao katika mabano nimshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (Agosti), beki wa Singida United, Shafiq Batambuze (Septemba) na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa (Oktoba). Wengine ni kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (Novemba), mshambuliaji wa Mbao FC ya Mwanza, Habibu Kiyombo (Desemba), mshambuliaji wa Simba, John Bocco(Januari), kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi (Februari), mshambuliaji wa  Lipuli, Adam Salamba (Machi) na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel Kaheza (Aprili).

Wachezaji hao kila mmoja amepewa zawadi ya tuzo, king'amuzi cha Azam na fedha taslimu sh. Mil. Moja kutoka kwa wadhamini Vodacom.

Hivyo wakati huu tukielekea mwisho wa ligi, leo tunatangaza wachezaji 30 ambao watawania tuzo hiyo, ambao watachujwa na kubaki 10, kisha watabaki watatu ambao ndiyo wataingia fainali ya kuwania tuzo siku ya mwisho.

Wachezaji hao 30 ni

1. Habibu Kyombo (Mbao)

2. Khamis Mcha- Ruvu Shooting

3. Yahya Zayd-Azam

4. Razack Abalora-Azam

5. Bruce  Kangwa-Azam

6. Aggrey Morris -Azam

7. Himid Mao –Azam FC

8. Awesu Awesu –Mwadui

9. Adam Salamba-Lipuli

10. Mohammed Rashid-Prisons

11. Shafiq Batambuze-Singida

12. Mudathir Yahya-Singida United

13. Marcel Kaheza- Majimaji

14. Ditram Nchimbi-Njombe Mji

15. Eliud Ambokile- Mbeya City

16. Shaaban Nditi-Mtibwa

17. Tafadzwa Kutinyu-Singida

18. Ibrahim Ajibu- Yanga

19. Gadiel Michael-Yanga

20. Papy Tshishimbi-Yanga

21. Kelvin Yondani-Yanga

22. Obrey Chirwa-Yanga

23. Aishi Manula-Simba

24. Emmanuel Okwi-Simba

25. John Bocco-Simba

26. Jonas Mkude-Simba

27. Erasto Nyoni-Simba

28. Shiza Kichuya-Simba

29. Asante Kwasi –Simba

30. Hassan Dilunga-Mtibwa

4 COMMENTS:

  1. Hapo wamemuacha Mlipili, kijana kaonesha kazi! Siyo mbaya lakini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dahh!! Jaman mlipili yko wap maonezi ayo

      Delete
    2. Dahh!! Jaman mlipili yko wap maonezi ayo

      Delete
  2. Hivi kweli unawezaje kumjumuisha Mtemea mate wenzie na kumuacha Kapombe? Ondoeni jina la Yondani muwekeni Dante. Nidhamu mchezoni Yondani hana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic