May 24, 2018



Baadhi ya mabalozi wa Dstv wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa  Kombe la Dunia kwa  lugha ya Kiswahili.




Wakali wa ving’amuzi nchini, kampuni ya Multichoice Afrika (Dstv) inazidi kuwa karibu na wateja wake baada ya juzi Jumatano kutangaza kuwa itaonyesha mubashara michuano ya Kombe la Dunia ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wote ulimwenguni.

Dstv wataonyesha mubashara mechi zote 64 za michuano hiyo mikubwa zaidi kwa upande wa timu za taifa kuanzia hatua ya makundi hadi mchezo wa fainali tena safari hii michuano hiyo itatangazwa kwa lugha ya Kiswahili.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa michuano hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Meneja Mwendeshaji wa Dstv, Baraka Shelukindo alisema kuwa wamekuja na kimbunga kwa safari hii ambapo wataonyesha michuano hiyo kuanzia awali hadi pale itakapofika tamati.


“Tumekuja na kimbunga kwa safari hii, tumedhamiria kuwapa raha wateja wetu hivyo wasubiri tu kupata ladha ya Kombe la Dunia kuanzia mwanzo hadi mwisho. Tofauti na watu wengine sisi tutaonyesha kila mchezo na hatutaruka hata mechi moja.

“Kwa kukidhi suala hilo wakati kombe hilo linaendelea kutakuwa na hadi chaneli sita ambazo zote zitakuwepo kwa ajili ya kukidhi haja ya mashabiki kutokukosa hata mchezo mmoja wa kombe hilo kubwa zaidi unapozungumzia juu ya timu za taifa.

“Lakini niwaambie kwamba mechi zote hizo zitakuwa zinaonyeshwa katika ubora wa juu kabisa (High Defination) yaani HD, tena kwa safari hii mashabiki watapata uhondo wa kombe hilo huku likitangazwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Tena kwa wakati huu kwa wateja wapya watapata ofa ya miezi miwili tu kwa kununua kifurushi cha Bomba kwa 79,000 huku wale wa zamani wenyewe kwa kupitia app yetu ya Dstv Now watakuwa na uwezo wa kuangalia sehemu yoyote ile kwa kutumia ipad, kompyuta bila ya hata kuwa nyumbani,” alisema Shelukindo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic