May 16, 2018


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo nchini Dkt. Harrison Mwakyembe, amewapongeza TBC na TV One kwa kufanikisha kuonyesha mechi 32 za Kombe la Dunia kwa bure kabisa.

Makyembe ameonesha kufurahishwa na uamuzi wa vituo hivyo vya runinga kuamua kuonesha mashindano hayo yatakayoanza mwezi Juni 2018 huko Russia.

Mbali na hayo, Waziri huyo mwenye dhamana ya michezo amevipongeza kwa kuonesha uzalendo kwa watanzania wanaosubiri burudani hiyo kwa hamu ambapo wataweza kutazama mechi hizo bure.

"Nimefuraishwa na uzalendo wa TBC na TV One kwa kuwapatia burudani Watanzani bure. Hiyo itasaidia pia televisheni hizo kujitangaza kimataifa na kupata matangazo"

Aliongeza, "Hivyo ni fursa kwa Watanzania sasa kupata ya bure kupitia muunganiko wa televisheni hizo mbili za TBC na TV One," alisema Mwakyembe katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia" alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic