May 24, 2018



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema bodi itakayoundwa kutoka upande wa wanachama ana wawekezaji, zote zitakuwa na lengo moja, kupata mafanikio kwa ajili ya klabu hiyo.

Akihojiwa leo, Hans Poppe amesema imekuwa kuna maneno yanayosambazwa kutaka kuonyesha kwamba hali ni mbaya na kutakuwa na ushindani au upinzani kati ya wale watakaotoka kwa mwekezaji yaani Mohamed Dewji na wale watakaokuwa wawakilishi wa wanachama.

“Hili jambo si sahihi, hawa wote ni Wanasimba. Kila watakachofanya kitakuwa ni kwa ajili ya kuiendeleza Simba na si vinginevyo.

“Kupishana kwa hoja ni jambo la kawaida kabisa. Lakini haina maana kwamba hawa wanataka kuvutana na hawa kwa lengo la kushindana au kuonyeshana.

“Ambacho watu wanapaswa kukumbuka hawa wote wanakuwa ni Wanasimba na si vinginevyo na watafanya lolote lengo likiwa ni kuiendeleza Simba,” alisisitiza.

Tayari Serikali imeridhia suala la mabadiliko ya katika ya klabu ya Simba na bilionea Mo Dewji amekubali kuwekeza kwa kumwaga Sh bilioni 20 ili apate hisa kwa asilimia 49 katika klabu hiyo na atakuwa mwekezaji mkubwa zaidi ya wengine na ataungana na wanachama wengine watakaonunua hisa zilizobaki kuwa wawekezaji.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic