May 24, 2018


Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, kimewasili Alhamis ya leo nchini kikitokea Mali kushiriki mchezo wa kuwania kufuzu fainali za vijana za AFCON (U20).

Ngorongoro wamerejea nchini baada ya kupoteza dhidi ya Mali kwa jumla ya mabao 6-2 uliopigwa jijini Bamako.

Kikosi hicho kiliweza kuruhusu mabao 2-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika hapa nchini kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam, kabla ya kwenda Mali na kuambulia kipigo kingine cha 4-1 na kufanya idadi ya mabao kuwa 6-2.

Kipigo hicho kimewaondoa moja kwa moja Ngorongoro Hereos kuwania tiketi ya kucheza mashindano hayo mwakani hivyo safari nyingine ya maandalizi itabidi ianze upya.


1 COMMENTS:

  1. Waache wawe wanyonge tu,sisi wapenzi wa soka Tanzania tulishakuwa wanyonge kabla wao hawajaziwa na tunaendelea kuwa wanyonge lakini kinachokera na unyonge zaidi ni pale watu wachache wanapofanya maamuzi ya hovyo kwa ghrama ya Watanzania wote.Mara ngapi wachezaji wenyewe na wadau wa mpira nchini kushsngazwa na maamuzi ya TFF wakati linapokuja suala la uteuzi wa makocha wa timu za Taifa. Kwa upande mwengine kwanini TFF wamepewa jukumu la kusimamia timu za Taifa? kwa maoni yangu hawana uwezo wa kuzisimamia hizi timu kwa maana ya kuziletea mafanikio ikiwa hata uteuzi wa makocha sahihi unawapa shida.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic