May 24, 2018


Klabu ya soka ya Alliance ya Mwanza iliyopanda Ligi Kuu Bara imeingia mkataba na Kocha Mnyarandwa, Baptista Kayiranga kwa ajili ya kuanza rasmi kazi ya kuinoa timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.

Kayiranga amewahi kuichezea klabu ya Rayon Sports inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda na Kombe la Shirikisho Afrika hivi sasa.

Kocha huyo pia aliweza kuiongoza Rayon kutwaa ubingwa wa ligi nchini Rwanda wakati akiwa mchezaji wa kikosi cha timu hiyo mwaka 2004.

Aidha, Kayiranga aliwahi kucheza soka la kulipwa katika moja ya klabu nchini Sudan akiwa kama kama winga wa kushoto.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic